Tuesday 3 February 2015

Leave a Comment

STORI YA KABINTI KAMOJA


Nilisoma naye chuo kimoja ( jina kapuni ), rafiki yangu alimpenda sana huyu msichana, but she was pretending to be in love with another man ( ambaye kwa mujibu wa taarifa za uhakika kutoka kwa watu wa karibu na huyu binti, walisha mwagana tangu enzi za pontio wa pilato and its like he was not existing ). Jamaa kwa kuwa alikuwa anamfeel huyu binti alienda naye hivyo hivyo kama mshika mapembe hadi tukamaliza chuo mwaka 2008. Binti alikuwa anampeleka sana jamaa, madesa yote yalikuwa ni wajibu wa jamaa, achilia mbali ishu za kumfanyia takehome tests and all that...Tumemaliza chuo, binti yupo mjini na jamaa yupo mjini but msimamo wa binti ulikuwa vilevile kwamba ana mtu wake toka zamani na wana mipango ya kufunga ndoa, jamaa kapiga sana simu katuma sana meseji hadi akachoka. Mwaka huo huo (2008) jamaa akapata FULLBRIGHT SCHOLARSHIP, akiwa marekani akatokea kupendana na dada mmoja chotara wa kizungu, wamefunga ndoa na sasa hivi wana mtoto mmoja. Kwa sasa jamaa ana fanya PHD kwenye chuo kimoja marekani ambako anaishi na familia yake...Mwezi uliopita alikuja kutembea home na kumtambulisha mke wake. He is no longer talking about that gal. Sasa kinacho nifanya nimshangae huyu binti, she is now blaming on us, anasema sisi ndo tumemshauri jamaa aachane naye, mara ooh jamaa alikuwa na maana gani kumtaka yeye kimapenzi halafu anakuja kuoa mwanamke mwingine!! I told her i dont have anything to do with that plus nikamuuliza kuhusu the so called mchumba wake na hakuwa na majibu yenye kueleweka but mwisho wa siku amejutia sana mambo yote aliyo mfanyia jamaa, alijaribu kumuomba msamaha, jamaa kamwambia yeye hana tatizo nae ila kuhusu uhusiano ndo hivyo tena,yeye tayari ni mume wa mtu. Anafikisha miaka 30 mwaka huu, hana mchumba wala bf, anauza dawa za GNLD ( U CAN SEE HOW DESPERATE SHE IS ). ....
KWENU MABINTI: Zile zama za SITAKI NATAKA , zimekwisha pitwa na wakati, do not pretend to be in love with someone else wakati unajua kabisa katika nafsi yako kwamba upo singo na unahitaji mwanaume..Kumbania mwanaume kwa muda mrefu hakuwezi kuongeza thamani yako hata kidogo

0 comments:

Post a Comment