Friday 2 January 2015

Leave a Comment

Mambo ya shanga hayoooo ucpimeeeeeeeeeeee

 

Dunia ni kubwa sana na ndani yake kuna walimwengu wanaoishi humo, ambao ni mimi na wewe na mara nyingi tumekuwa tukiishi kufuatana na wakati, ninaposema wakati namaanisha kuanzia mavazi, tabia na vitu vingine vingi ambavyo ndugu mdau wa page hii unaweza kuchangia.
Hapo awali wanawake wengi hasa wa kitanzania walikuwa wanapenda kuvaa shanga viunoni mwao, na wakati mwingine niliwahi kusimulia matumizi ya shanga, lakini kadri karne zinavyosogea watu wanabadilika kulingana na wakati.
hivi sasa wadada waliowengi hupenda kuvaa cheni viunoni mwao maarufu na pia kuna cheni nyingine huvaliwa kwenye mguu, na chen hizi huuzwa kwa gharama kubwa kwa sababu zimetengenezwa kwa madini ya ghari watu hupenda kuita (Vikuku) je unaweza kusema kazi yake nini hasa ya cheni hizi ambazo zimekuwa badala ya shanga? nataka maoni yenu wadau ili tujikumbushe kazi ya hizi cheni na kwa wale ambao hawajui wajue kupitia wewe mchangiaji!

0 comments:

Post a Comment