Thursday 5 March 2015

Leave a Comment

Bikira 2

Eti unaweza kumjua mwanamke bikira kwa kumwangalia jinsi anavyotembea! Kutokana na maandiko ya agano la Kale (Biblia) (Kumbukumbu la torati 22:13 17)
Wanaume wa kiisraeli walikuwa wanatahiriwa (circumcision) na hiki kitendo cha kutahiriwa au kukata govi (foreskin) kilikuwa ni agano (covenant) na Mungu wao, agano la damu kwa maana kwamba ubikira wa mwanaume ulitolewa kwa Mungu.
Hii ilikuwa na maana kwamba mwanaume sasa alikuwa ni mali ya Mungu (belong to God).
Kwa kutahiriwa damu ilitoka na damu kutoka ni kuonesha kutoa bikira na yeye kuwa na mahusiano na Mungu.
Mwanaume aliunganishwa na Mungu ambaye sasa anakuwa chanzo cha uwezo wake.
Agano la mwanaume na Mungu lilihitaji damu kutoka katika govi la uume na si katika sehemu nyingine ya mwili wa mwanamke kwa sababu uume ndiyo ulitumika pia kwa kuvunja kizinda (hymen) mwanamke kutoka damu kwa ajili ya agano kati ya mwanaume na mwanamke mbele za Mungu kuwa kitu kimoja.
Hii ina maana kwamba kwa mwanamke bikira kutoa damu ni muhuri wa agano kati ya mwanaume na mwamke mbele za Mungu.
Je, katika agano jipya bado tunahitaji damu ya binadamu kwa ajili ya agano?
Baada ya Yesu Kristo kuja yeye alitoa damu ya thamani msalabani ambao hutuunganisha wanadamu wote na Mungu.
Mwanaume na mwanamke wote wanaunganishwa na damu ya Kristo na wao kwa pamoja wanakuwa bikira (bibi harusi mtarajiwa) hadi siku Yesu akija kulichukua kanisa na kila mmoja ambaye atakutwa hana bikira maana ataachwa.
(Kama umeokoka utanielewa nazungumzia kitu gani)
Hivyo basi suala la msingi hapa si mwanamke kuwa bikira na kutoa damu ya agano kwa mume au mume kutahiriwa kutoa damu ya agano kwa Mungu bali kuikubali damu ya agano jipya ambayo ni Yesu Kristo.
Kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi ndiyo ubikira wa kweli
Je, inawezekana mwanamke bikira kuwa na mimba?
Ndiyo inawezekana, ikitokea sperms zinkawa deposited nje ya uke hata kama hakukuwa na penetrative sex kwani sperm ni genius au smart sana zikipata mwanya hasa kutokana na kufunguka kwa vitundu kwenye kizinda (hymen)
Je, ukiwa Bikira muda mrefu unaweza usizae watoto?
Uwongo mtu hasa kama mwanaume bado ana uwezo wa kuzalisha sperms na kama mwanamke bado anapata siku zake.
Je, unaweza kujua bikira kutokana na anavyotembea?
Thubuti! Hakuna external signal ambayo huweza kukufahamisha kama kweli mwanamke ni bikira au mwanaume ni bikira ukweli anajua yeye.
Je, Ukisubiri sex hadi uolewe au uoe ni mshamba kama si msenge?
Ukweli ni kwamba wewe ni smart sana kuliko wajinga wote wanaojiingiza kwenye masula ya sex kabla ya ndoa, Wazinzi na waasherati hawana nafasi katika ufalme wa Mungu.
Pia kusubiri kunakufanya uishi kwa amani na kutimiza malengo ya maisha bila hofu ya UKIMWI.
Je, Ukiwa in love na mtu lazima mfanye mapenzi?
Kuwa na mpenzi haina maana sex lazima, Pia inatokana na mipaka mliyowekeana.
Je, kwa mwanamke kudumisha urafiki na mwanaume sex ni muhimu?
Ukweli unajidanganya, kama urafiki wako ok shaky kiasi hicho kumbuka sex si tiketi ya kukufanya akupende zaidi bali tiketi ya kukupiga chini muda wowote na yeye kubeba kitu kipya kabisa.
Kama huamini nitumie email nitakupa mifano zaidi ya 100.

0 comments:

Post a Comment