Friday 2 January 2015

Leave a Comment

UJUE UONGO MTAMU KWENYE UHUSIANO


.

Kumbuka yapo mengi sana ambayo ukiongopa hayana madhara katika uhusiano
wako, lakini nimekuandalia yale ya muhimu zaidi.
Twende kazi.

IDADI YA WAPENZI: Nani amewahi kuwa mkweli kwa mpenzi wake
mpya kuhusu idadi ya mapatna aliowahi kutoka nao kimapenzi? Hebu anza na wewe mwenyewe?
Jiulize, tangu umeanza mapenzi umetoka faragha na wanaume/wanawake wangapi?
Je, upo tayari kumtajia mpenzi wako?

Umewahi kufanya hivyo? Rafiki zangu, kati ya mambo ambayo yanaudhi sana katika mapenzi, ni
pale mpenzi anapogundua kwamba mwenzi wake
ni ‘jalala’, yaani ametoka na wapenzi wengi kabla yake.

Wengi wanatamani sana kusikia kwamba wao ni wa pili au tatu, vinginevyo akutane na mwanamke
ambaye bado hajaanza kabisa mambo ya mapenzi.

Rafiki zangu, tuwe wakweli, kumwambia mpenzi wako kwamba umeshatoka kimapenzi na wanaume hamsini, ni sawa na kumtangazia kwamba wewe ni malaya.

Hata kama ni kweli umetoka na idadi hiyo,akikuuliza ipunguze, mwambie yeye ni mwanaume
wako wa nne! Wa kwanza,alikutoa usichana ukiwa mwanafunzi, baada ya hapo ukaachana naye kabisa na mapenzi.

Mwingine ulikutana naye chuo, ukamuacha baada ya kugundua kwamba alikuwa akipenda kukutumia tu, wa tatu ulifuma meseji ya mapenzi kwenye simu yake ukaamua kumuacha, yeye ni
wa nne!

Mwanaume huyo atajisikia fahari sana kuwa na mwanamke mwenye namba ndogo ya wanaume aliotembea nao, ingawa moyoni mwako unaujua ukweli, lakini inabidi udanganye ili kulinda penzi lako.

Tupo pamoja jamani?

UWEZO DUNI FARAGHA: Ukiwa na mpenzi wako, si ajabu sana katika
mazungumzo yenu ya kawaida, akakuuliza kuhusu uwezo wako wa kucheza ‘ligwaride’
muwapo faragha.

Kwa bahati mbaya kuna rafiki
wenye matatizo ya hapa na pale faragha.
Baadhi ya wanawake husumbuliwa na tatizo la maumivu wakati wa tendo, kuchelewa kufika mshindo na hivyo kuachwa njiani au kupoteza
hamu ya tendo.

Wanaume wao husumbuliwa na tatizo la kufika
mshindo mapema, kushindwa kurudia tendo na kuchoka mapema wakati mwenzake akiwa bado angali anamuhitaji.

Kimsingi matatizo makubwa hapa husababishwa
na utayari wa kisaikolojia, maandalizi duni n.k. Unapozungumza na mwenzako kuhusu hili,hutakiwi kumpa taarifa za kweli.
Zipo athari kadha wa kadha za kuwa mkweli juu ya matatizo
uliyonayo katika eneo hili.

Matatizo ya aina hii hutibiwa zaidi na mtu mwenyewe, kugundua udhaifu wake na kuufanyia
kazi.
Kama umegundua kwamba unapata maumivu wakati wa tendo, ni wazi kwamba maandalizi si ya kutosha, dawa yake hapo ni kutumia muda mwingi katika maandalizi kabla ya kuanza kazi yenyewe.

Kueleza tatizo lako moja kwa moja, kutamfanya mwenzako awe na mawazo, akiamini kwamba ama hutaendana na kasi yake, hatakufurahisha au
utamuacha njiani.

Kwa mtazamo huo ni rahisi sana
kufikiria kuachana na wewe ili akatafute anayeendana naye

0 comments:

Post a Comment