Friday 2 January 2015

Leave a Comment

UFANYE NINI UNAPOVUTIWA NA MPENZI MWENGINE.


Wapo watu ambao wameoa au wana wapenzi walioahidiana kwa mambo mengi, lakini wamekuwa wakikabiliwa na tatizo la kuvutwa kimahaba na watu wengine. Hali hii huwatokea wawapo masomoni, kazini, kwenye biashara,mbali au pengine hata karibu na wenza wao wa zamani.
Sayansi ya jamii inakubali kuwa mwingiliano wa kijamii mara nyingine huathiri tabia za watu,ukweli huu unathibitishwa na ongezeko la
usaliti katika mapenzi, mantiki ikibaki kwenye mwili kulazimishwa na mapokeo ya tafsiri ya vitu vinayotawala mawazo ya mwanadamu.
Maelfu ya wanaume na wanawake hulazimika kuwasaliti wapenzi wao baada ya kuvutiwa na maumbo au sura za wanaume/wanawake wanaokutana nao katika shughuli zao za kimaisha.
Wapenzi hao hujikwaa kupitia macho na hisia zao,huku wengi wakikiri kushindwa kuzuia matamanio
“Msichana/mvulana huyu ni mzuri sana nahisi kumpenda, nimuonapo nachanganyiwa kabisa.”
Inawezekana hata wewe unayesoma makala haya umewahi kutamka maneno haya na ukasahau kuwa umeoa/ umeolewa au una mchumba uliyepanga
kufunga naye ndoa.
Kama hilo halitoshi yawezekana umeshakuza mawazo hayo kiasi cha kuona huna jinsi zaidi ya kufanya
usaliti, ukatongoza au ukajitongozesha kwa gharama ili utii hisia zako.
Ninapotazama mwenendo wa wapenzi wengi siku hizi, nabaini kuwa mihemko ya miili inawaangusha wengi kwenye usaliti, jambo linalonifanya nilazimike
kufundisha namna ya kukabiliana na tatizo hili ili kuweza kuyanusuru mapenzi.
Naliita jambo hili tatizo kwa sababu limeleta madhara mengi katika jamii, kuna watu wameshauana, ndoa
kusambaratika na mapenzi kufa, isitoshe uchunguzi unaonyesha kwamba, wasaliti wengi hawakupata faida au raha waliyoitarajia kutoka kwa wale
waliowashawashi, hivyo kufanya hisia zao ziwe kazi bure.
Naamini hakuna mwenye akili timamu anayependa kupoteza utu wake bila faida. Ndiyo maana ipo
orodha ndefu ya watu walionifuata na kukiri: “Alinirubuni nikamwacha mpenzi wangu, kumbe alitaka kunichezea tu.”
Wanakiri kurubuniwa, lakini wanasahau kuwa walikubali baada ya kuvutwa na hisia!
Je mpaka sasa ni wanaume wangapi wanavutwa kimahaba na akidada warembo wanaokutana nao kiasi cha
kuwapuuza wapenzi wao wa zamani na kuamua kuwasaliti?

0 comments:

Post a Comment