Friday 2 January 2015

Leave a Comment

UTUNZAJI WA MATITI WAKATI WA HEDHI NA UJAUZITO




Natambua kuwa uvaaji wa sidiria wakati matiti yanakua, wakati wa hedhi na wakati wa ujauzito ni karaha sana na unahisi kubanwa tu (kwa vile yanauma kiaina) na hali hiyo hufanya wengi kuachana nazo na kuachia matiti yakining'inia bila "support".

Kama nilivyosema awali kuwa matiti wakati wa hedhi huongezeka ili kuwa tayari kutengeneza chakula cha mtoto ambae kwa wakati huo yai lako linakuwa likisubiri kurutubishwa na mbegu ya kiume lakini hilo lisipotokea basi matokeo yake ni wewe kupata hedhi.

Si wanawake wote wanaopata maumivu/ongezeko la ukubwa wa matiti wakati wanakaribia hedhi na wakati wa hedhi, lakini ikiwa wewe ni mmoja ya wale ambao matiti huongezeka ukubwa unapokaribia na wakati wa hedhi basi hakikisha unafanya mazoezi kama niliyoeleza kule mwanzo na pia zingatia kuvaa sidiria wakati wote isipokuwa wakati wa kulala.

Vilevile kwa wamama wajawazito ni vema kuvaa sidiria ili kuyasaidia uzito wa matiti yako usiyavute kwenda chini hali itakayopelekea kuwa na matiti yaliyolala mara baada ya kujifungua.


Vaa sidiria au vest kadili siku zinavyo kwenda!


Jinsi matiti yanavyokuwa ndio uzito wake huongezeka hivyo kama binti/mwanamke unahitaji kuyasaidia kwa kuvaa kitu ambacho kitayasaidia kubaki pale yanapopaswa kubaki......nina maana vaa sidiria.

Vest ivaliwe wakati ukifanya mazoezi au unaweza kujifunga khanga (nyepesi) chini ya matiti yako hali itakayosaidia matiti yasiume sana wakati unafanya unayasumbua(inategemeana na ukubwa wake).

Wakati nakuwa wanawake wengi walikuwa wakiamini kuwa kuvaa sidiria kunasababisha matiti kuanguka; sio kweli.

Kumbuka kutovaa sidiria wakati wa kulala kwani naweza kusababisha uvimbe (damu kujikusanya pamoja) ktk matiti yako na badala yake lala kifudifudi(lalia matiti yako a.k.a lalia tumbo) ili kuya-support.

0 comments:

Post a Comment